Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Mufti Muhammad Taqi Othmani, mwanachuoni mashuhuri wa Kisunni nchini Pakistan na mkuu wa taasisi ya kielimu ya Darul Uloom Deoband, kupitia ujumbe aliouchapisha katika akaunti yake kwenye mtandao wa kijamii "X" (zamani Twitter), alionesha radi amali yake dhidi ya uvamizi wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran.
Katika ujumbe huo alisema:
"Jibu thabiti la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limeonyesha kuwa Iran inatoa majibu yenye nguvu dhidi ya Israel, na hii ni mara ya kwanza Israel inahisi ladha ya kweli ya mabomu."
Ingawa Iran imepata baadhi ya hasara kufuatia uvamizi huo, lakini imejibu kwa nguvu na kwa uthabiti. Leo hii, Israel kwa mara ya kwanza imeelewa maana halisi ya kushambuliwa kwa mabomu. Malengo ya chuki ya utawala huu dhidi ya ulimwengu wa Kiislamu hayafichiki kwa yeyote.
Tukio hili ni fursa nyingine iliyotolewa na nguvu ya Mwenyezi Mungu kwa umma wa Kiislamu ili, kwa mshikamano kamili, wasimame imara mbele ya vitisho vya utawala wa Kizayuni na wauweke kabisa chini ya udhibiti.
Maoni yako